Wakati unatutupa mkono kukabili ukame Kusini mwa Afrika:FAO

Wakati unatutupa mkono kukabili ukame Kusini mwa Afrika:FAO

Pakua

Zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kuanza kuandaa mashamba kwa ajili ya msimu mwingine kilimo, watu milioni 23 Kusini mwa Afrika wanahitaji msaada.

Kwa mujibu wa shirika la kilimo na chakula FAO msaada huo ni wa kuzalisha chakula cha kutosha kujilisha wao wenyewe.

Hii ni kutokana na hali mbaya ya ukame unaolikumba eneo hilo ukichangiwa na El Nino. Shirika hilo linasema endapo msaada huo hautapatikana sasa kutoka kwa wahisani basi kutakuwa na ongezeko kuibwa la nchi hizo kutegemea msaada wa kibinadamu hadi katikati yam waka 2018.

Kufafanua zaidi ni Neil Marsland afisa wa masuala ya kiufundi FAO kitengo cha operesheni za dharura.

(SAUTI YA NEIL MARSLAND)

Photo Credit
Mkulima anapumzika huko Swaziland. Picha: FAO / Rodger Bosch