Kampeni dhidi ya kipindupindu inaendelea Sudan Kusini:WHO

Kampeni dhidi ya kipindupindu inaendelea Sudan Kusini:WHO

Pakua

Juhudi za kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu Sudan Kusini zimeimarishwa kwa mujibu shirika la afya ulimwenguni WHO.

Taifa hilo change kabisa duniani limeorodhesha visa 270 vya kipindfupindu, vikiwemo vifo 14 tangu Julai 12. Kwa pamoja wizara ya afya ya Sudan Kusini, WHO na washirika wake, wiki hii wamezindua chanjo ya kipindupindi ili kuwafikia watu zaidi ya 14,000.

WHO pia imeanzisha kituo cha tiba ya kipindupindu kwenye mji mkuu Juba , na inajitahidi kuimarisha uwezo wa kukabiliana na ugonjwa huo.

Kipindupindu ni ugonjwa unaoambatana na kuhara kupindukia na hivyo kusababisha wagonjwa kuwa na upungufu wa maji mwilini, na usipotibiwa haraka na ipasavyo husababisha vifo.

Photo Credit
Msichana akipokea chanjo ya kipindupindu.Picha:UN Picha / JC McIlwaine