Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Thailand yatakiwa kuhakikisha mjadala huru kabla ya kura ya maoni ya katiba:UM

Thailand yatakiwa kuhakikisha mjadala huru kabla ya kura ya maoni ya katiba:UM

Pakua

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza, David Kaye, leo amelaani idadi kubwa ya watu kukamatwa na kufunguliwa dhidi ya umma na mitandao ya kijamii, vilivyoletwa na sheria za kijeshi na sharia ya kura ya maoni ya katiba ya Thailand.

Sheria hiyo iliyopitishwa kabla ya kura ya maoni ya katiba hapo Agosti 7, inaharamisha kujieleza na fursa ya kupata taarifa kuhusu mswada wa katiba.

Tangu Juni mwaka huu kumeripotiwa kwamba watu 86 wanachunguzwa au wamefunguliwa mashitaka katika msako wa serikali wa kupaza sauti kabla ya kura ya maoni ya Agost 7.

Wanaharakati kadhaa wamekamatwa mapema mwezi huu chini ya sharia mpya ya kura ya maoni kwa kufanya kampeni na kuwachagiza wapiga kura kuukataa mswaada wa katiba.

Photo Credit
David Kaye. (PICHA:UN/Jean-Marc Ferré)