Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSCA yakaribisha kuachiliwa kwa mateka wa Cameroon

MINUSCA yakaribisha kuachiliwa kwa mateka wa Cameroon

Pakua

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, umekaribisha kuachiliwa hapo Julai 17, kwa mateka 11 waliosalia raia wa Cameroon, ambao walikuwa wanashikiliwa na kundi la Democratic Front for the Central African People (FDPC).

Mateka hao walikabidhiwa kwa uongozi wa Cameroon baada ya miaka zaidi ya miwili na nusu matekani.

MINUSCA pia imetoa wito wa kuachiliwa meya na waumini wa Baboua ambao bado wanashikiliwa na FDPC tangu Julai 16 mwaka jana, licha ya wito unaotolewa mara kwa mara wa kutaka waachiliwe.

MINUSCA imerejelea wito wake kwa makundi yote yenye silaha kuacha machafuko bila masharti yeyote na kujiunga na mchakato wa majadiliano ulioanzishwa na serikali ili kuimarisha usalama na kujenga taifa endelevu.

Photo Credit
Walinda amani wa MINUSCA wapiga doria nchini CAR.(Picha:UM/Nektarios Markogiannis)