Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuongeze kasi ya utekelezaji ili kufikia SDG’s -Eliasson

Tuongeze kasi ya utekelezaji ili kufikia SDG’s -Eliasson

Pakua

Nchi zinapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs, endapo dunia inataka kufikia malengo hayo muhimu.

Hayo ni kwa mujibu wa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, akiwahutubia mawaziri wanaohudhuria kongamano la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu leo Jumatatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Kongamano hilo litakuwa likifanyika mara kwa mara , ili kuhakikisha kwamba malengo hayo yaliaofikiwa Septemba mwaka jana yanajojumuisha kutokomeza umasikini ifikapo 2030 yanafikiwa.

Bwana Eliasson amesema haitakuwa kazi rahisi kwenda na kazi ya utekelezaji lakini ameahidi kwamba Umoja wa Mataifa utazisaidia nchi katika juhudi zao.

(SAUTI YA ELIASSON)

"Ni muhimu kuhakikisha hakuna atakayesalia nyuma, suala ambalo ni kitovu cha ajenda ya mwaka 2030, na ni kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu. Endapo tutashirikiana kwa pamoja, kote ndani na miongoni mwa mataifa, tukusanye nguvu kwa pamoja tunaweza kufikia na kuwa na dunia bora yenye amani, fursa na hadhi kwa wote”

Photo Credit
Jan Eliasson. Picha ya UN/Evan Schneider