Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pengo baina ya misitu na kilimo lizibwe kuimarisha uhakika wa chakula:FAO

Pengo baina ya misitu na kilimo lizibwe kuimarisha uhakika wa chakula:FAO

Pakua

Shirika la Umoja wa mataifa la chakula la kilimo FAO leo Jumatatu limetoa ripoti kuhusu hali ya misitu duniani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo  kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya chakula duniani kutahitaji ardhi yenye rutuba na uzalishaji endelevu.

Ripoti hii pia inafafanua ni jinsi gani na kwa nini sekta ya misitu inajukumu kubwa kwa uzalishaji wa chakula duniani. Pia imetaja nchi 22 ambazo zimefanikiwa kupanuia wigo wa eneo la misitu ili kuboresha uhakika wa chakula.

Photo Credit
Mtoto anayepanda miti nchini Haiti. Picha ya Umoja wa Mataifa/Logan Abassi.