Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa inaweza kutoepukika Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Njaa inaweza kutoepukika Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Pakua

Njaa inaweza kutoepukika katika maeneo yaliyoathirika zaidi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria , tathimini ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada imeonyesha.

Misafara ya misaada imebaini kiwango cha juu cha utapia mlo na hali kama ya baa la njaa kwenye jimbo la Borno , hususani kwenye makambi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.

Makambi haya hayana usalama, na ni vigumu kuyafikia, na mengi yapo katika maeneo ambayo machafuko yanaendelea. Wanamgambo wa Boko Haram wamefanya mashambulizi mengi katika wiki za karibuni , na kuwatawanya maelfu ya watu kwenye eneo la bonde la ziwa Chad.

Kwa mujibu wa OCHA dola milioni 221.6 zinahitajika ili kukabiliana na mahitaji ya haraka ya kibinadamu kati ya sasa na mwezi Septemba.

Photo Credit
Watu waliokimbia makwa o nchini Nigeria.(Picha:Maktaba/OCHA/Jaspreet Kindra.)