Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni hatua kubwa kufikisha misaada kulikozingirwa:Egeland

Ni hatua kubwa kufikisha misaada kulikozingirwa:Egeland

Pakua

Kufikishwa kwa msaada katika maeneo mawili ya mwisho yaliyozingirwa Syria, ambayo hajakuwa na msaada wowote kutoka nje tangu 2012 kunadhihirisha hatua kubwa kabisa ya kibinadamu umesema Alhamisi Umoja wa Mataifa.

Ujumbe huo ni kutoka kwa Jan Egeland, mratibu wa kikosi kazi cha kimataifa cha masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa mjini Geneva baada ya misaada ya kibinadamu kuwasili maeneo ya Arbin na Zamalka vijijini Damascus.

Licha ya kukaribisha hatua hiyo muhimu Engeland Egeland aelezea hofu yake ya hatari ya watu kufa njaa katika maeneo mengine pia ugumu uliopo katika kufikisha misaada kwa wakimbizi wanaoihitaji.

Kuwasili kwa misaada hiyo Egeland amesema inamaanisha sasa maeneo yote 18 yanayozingirwa kwa mujibu wa Umoja wa mataifa sasa yamefikiwa.

Photo Credit
Watoto kutoka Yarmouk. UNRWA/Rami Al-Sayyed