Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yalaani uharibifu dhidi ya vituo vya afya Libya

WHO yalaani uharibifu dhidi ya vituo vya afya Libya

Pakua

 

Shirika la afya ulimwenguni WHO limelaani mashambulizi ya hivi karibuni katika vituo viwili vya afya mjini Benghazi nchini Libya ambayo yameelezwa kusababisha uharibifu kwa majengo na vifaa tiba.

Taarifa ya WHO inasema kuwa mnamo Juni 21 roketi ilipiga paa lililokarabatiwa mwaka 2014 baada ya shambulizi wakati wa machafuko mwaka 2011.

Kituo hicho cha afya kilichoshambuliwa kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 300 na zaidi ya watu 400 walikuwepo kwenye kituo hicho wakati wa shambulio , ambapo uharibifu katika chumba cha upasuaji umesababisha kusimama kwa  huduma hatua iliyolazimisha wagonjwa kuhamishiwa katika kituo jirani.

WHO imeeleza kuwa katika shambulio jingine la Juni 22, jengo la utawala la kituo cha afya Benghazi  liliharibiwa vibaya baada ya gari kulipuka katika eneo la kuegesha magari.

Hata hivyo hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa  katika mashambulizi hayo.

Photo Credit
Raia wa Libya wakiandamana nchini Libya mwaka 2011 kuomba jeshi la kitaifa lirejeshe hali ya usalama. Tangu mwisho wa vita vya 2011, utawala wa sheria haujarejeshwa kikamilifu nchini humo, kwa mujibu wa watalaam wa Umoja wa Mataifa. Picha ya UN/Iason Foou