Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande kinzani Yemen zina wajibu wa kimaadili na kisiasa.

Pande kinzani Yemen zina wajibu wa kimaadili na kisiasa.

Pakua

Pande kinzani katika mgogoro wa Yemen zina wajibu wa kimaadili na kisiasa katika kusitisha machafuko amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jumapili.

Akiongea nchini Kuwait ambapo majadiliano ya upatanishi yamekuwa yakifanyika Ban ameelezea kusikitishwa kwake na hali tete katika eneo la mapigano.

Katibu Mkuu ambaye pia amekutana na mamlaka za mataifa ya Uajemi na kuwashukuru kwa usaudizi wao katika mchakato wa kusaka amani nchini Yemen, pia amezionya pande kinzani kuwa hakuna muda wa kupoteza.

Amesema hali inazidi kuwa tete kila uchao na mgogoro unavyozidi kufukuta ndivyo muda wa kurejelea utulivu unavyozidi kuongezeka

(SAUTI BAN)

 ‘‘Kuna ukosefu mkubwa wa chakula, uchumi uko katika segemnege. Wakati ukomeshwaji wa uhasama unasuasua, kumekuwa na uhalifu mkubwa unaosababisha majeruhi na madhila kwa raia wakiwamo watoto. Hali hii ya kuogofya inawapa enyi wajumbe wa majadiliano jukumu kubwa. Muna wajibu wa kimaadili na kisiasa.’’

Ban amezitaka pande kinzani kurejelealea mchakato wa mpito ulioanzishwa mwaka 2011.

Mapigano kati ya serikali na kundi la waasi la Houthi  yamesababisha zaidi ya watu milioni 2.4 kulazimika kukimbia makwao.

Photo Credit