Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada kwa watu 150,000 wa Syria kusafirishwa kwa ndege:WFP

Msaada kwa watu 150,000 wa Syria kusafirishwa kwa ndege:WFP

Pakua

Msaada wa chakula unaohitajika haraka kusaidia watu 150,000 utasafirishwa kwa ndege hadi Kaskazini Mashariki mwa mji wa Qamishli Syria ambako chakula kimekwisha umesema leo Umoja wa Mataifa.

Akitangaza maendeleo hayo afisa wa mipango wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Bettina Luescher amesema hali ni mbaya hasa kwenye jimbo la Hasakeh .Jimbo hilo halijapata msaada wowote kwa njia ya barabara tangu mwanzoni mwa 2014. Akiongeza kwamba anatumai serikali ya Syria itakubali ujumbe huo wa msaada siku chache zijazo.

(SAUTI YA BETTINA)

“Wiki iliyopita tulikuwa tuliwapa mlo wa mwisho watu zaidi ya 5,300 peomjini Qamishli, hivyo tumeishiwa akiba kabisa ya chakula kilicho tayari kuliwa na hapo kabla akiba ya mgao wa kawaida wa chakula ulimalizika."

Ingawa ni gharama kubwa usafirishaji kwa ndege wa chakula unaendelea kwa sababu , wanamgambo wa ISIS wanadhibiti barabara kuelekea Hasakeh kutoka maeneo jirani ya majimbo ya Raqqa na Deir-Ez-Zour.

Shughuli hiyo itaratibiwa na WFP na kufungua mlango kwa mashirika mengine ya Umoja wa mataifa na washirika wake.

Photo Credit
Usambazaji wa msaada wa chakula nchini Syria.(Picha:WFP)