Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UK nje ya muungano wa Ulaya, Ban aahidi mshikamano na pande zote

UK nje ya muungano wa Ulaya, Ban aahidi mshikamano na pande zote

Pakua

Sasa ni rasmi Uingereza imeamua kujiengua kutoka Muungano wa Ulaya kupitia sauti ya wengi, kura ya maoni.

Akizungumzia matokeo hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema amefuatilia kwa karibu mjadala mzima na uamuzi wa kujitoa umekuja baada ya mjadala na mchakato mzito sio tu kwa Uingereza bali kwa Ulaya nzima.

Amesema sasa Uingereza na nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya wanaanza mchakato wa nini kitakachofuata na kwa hilo Ban amesema anaiamini historia ya Ulaya na uwajibikaji wao kwa maslahi ya raia wake.

Kwenye Umoja wa mataifa Ban amesisitiza unatarajia kufanya kazi kwa karibu na pande zote , Uingereza na Muungano wa Ulaya kwani wote ni washirika muhimu.

Pia ameziomba pande zote kuendelea na ushirika wao na Umoja wa Mataifa katika maendeleo, masuala ya kibinadamu na amani na usalama ikijumuisha suala la wahamiaji.

Photo Credit
Bendere za Uingereza na EU:Picha na UM