Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM ataka kampuni binafsi ziwezeshe uhuru kwenye mitandao ya intaneti

Mtaalam wa UM ataka kampuni binafsi ziwezeshe uhuru kwenye mitandao ya intaneti

Pakua

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kuwa na maoni na kujieleza, David Kaye, anazindua wiki hii mchakato wa kutathmini wajibu wa kampuni za kibinafsi katika kuhakikisha uhuru huo unaendelezwa kwenye mitandao ya intaneti.

Akiwasilisha ripoti yake kwa Baraza la Haki za Binadamu jijini Geneva, Bwana Kaye amesema kampuni za kibinafsi hufanya uamuzi unaoathiri kwa kiasi kikubwa uhuru wa kujieleza kwenye intaneti.

Mtaalam huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ni jambo la kawaida kwa kampuni binafsi kubinya, kufuatilia, au kuweka vizuizi dhidi ya uhuru wa kujieleza, hususan zinapopata shinikizo kutoka kwa serikali, lakini wakati mwingine zinafanya hivyo zenyewe bila shinikizo.

Amesema kampuni zinahitaji mwongozo kuhusu jinsi viwango vya haki za binadamu vinavyowezesha kazi yao kama walinzi wa haki, na wawezeshaji wa haki ya kujieleza, akitaja baadhi ya vitendo vinavyobinya uhuru wa kujieleza mitandaoni, mathalani kukata huduma za mawasiliano kupitia mitandaoni, kuifunga mitandao kwa kisingizio kwamba inatumiwa kueneza itikadi kali na kauli za kuzua chuki, au kuendeleza kile kinachotajwa kuwa maadili ya jamii.

Photo Credit
UN Photo/Devra Berkowitz