Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za misaada zimepigwa Syria licha ya kuendelea kwa vita

Hatua za misaada zimepigwa Syria licha ya kuendelea kwa vita

Pakua

Nchini Syria hatua zimepigwa katika kufikisha misaada inayohitajika haraka umesema Alhamisi Umoja wa Mataifa kabla ya kuonya kwamba fursa ya kufanya hivyo inaweza kutoweka kesho kufuatia mapigano.

Jan Egeland, anayeratibu kikosi kazi cha kimataifa cha misaada hiyo ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Geneva, amesema maeneo 16 kati ya 18 yanayozingirwa yamepokea msaada tangu mwezi Februari ikilinganishwa na maeneo mawili tu mwaka jana.

Hadi mwisho wa siku ya leo , Umoja wa Mataifa na washirika wake wanatumai kuwafikia watu 110,000 katika maeneo yanayozingirwa wakiwa na malori 100 yaliyosheheni msaada.

Wakati akikaribisha habari za kusitisha uhasama kwa saa 48 mjini Aleppo, Bwana Egeland ametoa wito wa usitishaji mapigano zaidi

(SAUTI YA EGELAND)

“Yote haya yanatokea wakati mapigano yamekuwa mabaya zaidi, mabomu yamezidi, na mahitaji ya ulinzi kwa raia yamezidi kukanganyika kote nchini Syria.”

Photo Credit
Wakimbizi wa ndani Syria wakipokea msaada. Picha ya UNRWA.