Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Rais wa Baraza la Ulaya, wajadili SDGs, ugaidi, wakimbizi

Ban akutana na Rais wa Baraza la Ulaya, wajadili SDGs, ugaidi, wakimbizi

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Ulaya (EU), Donald Tusk.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wake kufuatia mkutano huo imesema Ban ameusifu Muungano wa Ulaya kwa uungaji wake mkono maadili ya Umoja wa Mataifa, na kwa uongozi wake katika kuridhia na kutekeleza ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Mkataba wa Paris kuhusu mabdailiko tabianchi.

Aidha, Katibu Mkuu amemshukuru Rais Tusk kwa uungaji mkono wa EU kwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua za kuzuia itikadi kali katili, huku akikumbusha haja ya ushirikiano imara wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

Halikadhalika, Ban ameshukuru juhudi za EU katika kudhibiti mmiminiko mkubwa wa wahamiaji na wakimbizi barani Ulaya, ikiwemo kupitia kufungua njia za kisheria za watu kuhamia Ulaya.

Photo Credit
Ban Ki-moon, alipokutana na Rais wa Baraza la Ulaya (EU), Donald Tusk.(Picha:UM/Rick Bajornas)