Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila kupunguza umasikini hatutaweza kukabiliana majanga: Glasser

Bila kupunguza umasikini hatutaweza kukabiliana majanga: Glasser

Pakua

Ili kukabiliana na majanga lazima kupunguza umasikini amesema mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR Bwana Robert Glasser.

Katika mahojiano na idhaa hii wakati wa mkutano nchini Paraguay uliojumuisha mataifa yote ya Amerika kuhusu jinsi gani ya kutekeleza makubaliano ya kimataifa ya kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na majanga ya asili, amesema maeneo mengi yenye umasikini hukabaliana na majanga.

Akitolea mfano amesema.

( SAUTI ROBERT)

‘‘Ukanda huu una asilimia 20 ya watu wanaoshi katika maeneo ya pembezoni mjini Shante. Sehemu hizi mara nyingi zi karibu na milima kunapotokea maporomoko au mafuriko. Wakati mwingine ukanda wa Pwani ulio hatarini kukumbwa na dhoruba’’

Amesema kampeni ya kuounguza majanga lazima ijikite zaidi katika kupunguza umasikini vinginevyo kazi ya msingi haitofanikiwa.

Photo Credit
Robert Glasser.UN Radio/C. Garcia