Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi zenye hadhi ni muhimu katika kupunguza umasikini: Bi Oliphant

Kazi zenye hadhi ni muhimu katika kupunguza umasikini: Bi Oliphant

Pakua

Wakati wiki ya kwanza ya mkutano wa kimataifa wa 105 wa masuala ya kazi ikielekea ukingoni, mwenyekiti wa mkutano huo, waziri wa kazi wa Afrika ya Kusini Bi Mildred Oliphant, amesema kazi zenye hadhi ni muhimu sana katika kupunguza umasikini.

Amesema mamilioni ya watu hasa barani Afrika wanatumbukia kwenye ufukara kutokana na kukosa ajira za maana, akieleza jinsi masuala hayo yanavyojitokeza nchini mwake na Afrika nzima kwa ujumla

(OLPHANT CUT 1)

‘Barani Afrika ikwa wewe ndiye unaleta mlo kwenye kaya, husaidii kaya yako pekee bali ndugu na jamaa. Kwa mfano nafanya kazi na nasaidia familia ya watu sita. Lazima uangalie ni familia ngapi nyingine zenye watu sita ambazo nazisaidia.’’

Pia katika suala la usawa wa kijinsia kazini na kuhakikisha wanawake hawaachwi nyuma katika ajenda hii ya kazi zenye hadhi akitoa mfano wa nchi yake Bi Ophant anasema

(OLPHANT CUT 2)

‘‘Tuna sheria ambayo inazungumzia usawa katika ajira. Inasema kila mtu ni sawa, na ikija katika ajira kila mtu anapaswa kuajiriwa bila kuzingatia jinsia yake. Pia malipo sawa kwa kazi zenye thamani sawa.’’

Photo Credit
Picha ya ILO.