Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa China barani Afrika kubadilika ili kuleta maendeleo endelevu

Uwekezaji wa China barani Afrika kubadilika ili kuleta maendeleo endelevu

Pakua

Uwekezaji wa kampuni za kichina kwenye uchumi wa Afrika huenda ukaleta ajira na ukuaji wa uchumi endelevu zaidi, iwapo utalenga sekta zenye tija zaidi.

Huo ulikuwa ni ujumbe wa Arancha Gonzales, Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha biashara ya kimataifa ITC kwenye Kongamano la Uwekezaji wa China kwa ajili ya biashara na ukuaji uchumi endelevu barani Afrika lililofanyika leo mjini Beijing.

Taarifa ya ITC imeeleza kwamba bwana Gonzales amependekeza wawekezaji wachina wasaidie sekta ya usindikaji mazao na viwanda vidogo ili kuzalisha thamani na ajira zaidi pamoja na kujengea uwezo wa kampuni ndogo na za kati kuuza bidhaa zao nje.

Aidha amekumbusha kwamba bara la Afrika ndilo la pili duniani kwa ukuaji wa uchumi na uwekezaji wa kimataifa, akionyesha kwamba China imeongeza maradufu kiwango cha uwekezaji barani humo kwa kipindi cha miaka kumi.

Hata hivyo bwana Gonzales ameonyesha kwamba uwekezaji huo wa kichina umelenga zaidi sekta za nishati, usafiri na madini, akiongeza kwamba sekta zingine kama usindikaji wa mazao ya kilimo ya viwanda vidogo zingeweza kusababisha maendeleo endelevu zaidi.

Photo Credit
Picha:ICT