Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wengine 700 wahofiwa kufa maji wakielekea Ulaya

Wahamiaji wengine 700 wahofiwa kufa maji wakielekea Ulaya

Pakua

Takribani wahamiaji 700 wanahofiwa kufa maji baada ya  kuzama  kwa boti walizokuwa wanasafiria katika pwani ya Libya mwishoni mwa juma lililopita wakati makundi hayo yakijaribu kuhamia Ulaya kwa vyombo visivyo salama.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limethibitisha taarifa hizo.

Hali ya hewa imesababisha upotevu wa amisha ya maelfu ya wahamiaji kutok Afrika wanaokimbilia Ulaya.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa  msemaji wa UNHCR William Spindler  ametoa wito wa kusaidia kukomesha vifo hivyo vinayoendelea.

(SAUTI SPINDLER)

‘‘Tunazitaka mamlaka barani Ulaya na duniani kote, kusaidia zaidi nchi ambazo hawa wakimbizi wanatoka, nchi ambazo ni wenyeji wa wa idadi kubwa ya wakimbizi.’’

Photo Credit
Wahamiaji wakiwa hoi taabani baada ya kutembea siku kadhaa. Hapa ni katika kituo cha polisi cha Rozke nchini Hungary. (Picha:© UNHCR/B. Baloch) (MAKTABA)