Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa yahimizwa kuangazia tishio la ADF,DRC

Jamii ya kimataifa yahimizwa kuangazia tishio la ADF,DRC

Pakua

Wawakilishi wa mkakati wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na ukanda wa Maziwa Makuu (PSC) wamesihi Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO na jeshi la kitaifa FARDC kuimarisha ushirikiano wao katika kupambana na waasi wa ADF.

Wametoa salamu zao za rambirambi kwa familia za wahanga wa mashambulizi ya waasi hao wakipongeza jitihada za FARDC. Aidha wamewaomba raia kuendelea kushirikiana na askari wa MONUSCO na FARDC.

Taarifa hiyo ya pamoja imetolewa leo baada ya ziara ya wajumbe hao kwenye eneo la Beni, mashariki mwa nchi, lililokumbwa na mashambulizi ya ADF.

Kwenye ziara hiyo wamejadiliana na viongozi wa MONUSCO na FARDC ambao wanaoongoza kwa pamoja operesheni USALAMA dhidi ya ADF.

Kwa mujibu wa taarifa yao, wajumbe hao ambao wanawakilisha Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika na mashirika ya kikanda wamepokea malalamiko ya jamii na viongozi wa serikali za mitaa ambao wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu mauaji ya raia yanayofanyika licha ya uwepo wa MONUSCO na FARDC, wakiiomba jamii ya kimataifa kuongeza bidii ili kulinda raia.

Photo Credit
UN Photo/Clara Padova