Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki-limbukeni

Neno la wiki-limbukeni

Pakua
Ijumaa ya tarehe 16 Mei mwaka 2016 tuliangazia matumizi ya neno limbukeni. Mtaalamu wetu alikuwa Onni Sigalla, mhariri mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.
Bwana Sigalla anaangazia neno limbukeni ambapo anafafanua limbukeni kama mtu ambaye anapata kitu kwa mara ya kwanza aghalabu kitu chenye thamani na kuonyesha kukiajabia sana. Aidha ni mtu ambaye anafanya kitu kwa mara ya kwanza na kupata shida kwa sababu hana mazoe nacho.
Photo Credit