Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujuzi wa asili wafaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi: Watu asilia

Ujuzi wa asili wafaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi: Watu asilia

Pakua

Njia za asili zaweza kutumiwa kisayansi katika kukabilina na mabadiliko ya tabianchi, amesema mwakilishi wa jamii ya watu wa asili ya Kimasai kutoka Tanzania Martha Ntoipo.

Katika mahojiano na idhaa hii kandoni mwa mikutano kuhusu jamii ya watu wa asili inayojadili mambo kadhaa ikiwamo mabadiliko ya tabia nchi mjini New York, Bi Ntoipo amesema jamii asilia ina ujuzi asili wa kunga’mua hali ya hewa kwahiyo.

( SAUTI)

Hapa anatoa mfano wa kutambua hali ya hewa kwa kutumia mbalamwezi.

Photo Credit
Picha: Kiswahili Radio/UM