Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa UM kukabiliana na Zika wazinduliwa

Mfuko wa UM kukabiliana na Zika wazinduliwa

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameanzisha mfuko wa Umoja wa Mataifa kukabiliana na Zika unaohusisha wadau mbalimbali (MPTF) ili kufadhili masuala muhimu ya kipaumbele katika kupambana na mlipuko wa Zika.

Mfuko huo unatoa mfuko huo wa wa dhamana unatoa haraka, kwa urahisi na jukwaaa la kuwajibika katika kusaidia kuchukua hatua haraka kutoka kwa Umoja wa mataifa na wadau wengine pindi uzukapo ugonjwa huo.

Fedha za haraka zinahitajika ili kusaidia utekelezaji wa mipango ya kitaifa na kushughulikia changamoto za kiuchumi na kijamii zijazo.Mfuko huo wa kukabiliana na Zika MPTF , utasaidia moja kwa moja mikakati ya Zika iliyowekwa na shirika la afya duniani WHO , kwa kujadiliana na mashirika ya Umoja wa mataifa, washirika, na wataaalamu wa kimataifa.

WHO inasema virusi vya Zika vinasambaa haraka, tangu Januari 2015 nchi na himaya 51 ziearifu maambukizi ya virusi vya Zika. Mkakati wa Zika una lengo la kuchunguza na kukabiliana na matatizo ya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo microcephaly na matatizo mingine ya mishipa yanayohusishwa na virusi vya Zika.

Photo Credit
IAEA kwa ushirikiano na FAO wanafanya utafiti juu ya mbinu za kukabiliana na mbu.(Picha:D. Calma/IAEA)