Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kanuni mpya za uhamiaji Ulaya zilinde haki za watoto- UNICEF

Kanuni mpya za uhamiaji Ulaya zilinde haki za watoto- UNICEF

Pakua

Wakati Umoja wa Ulaya ukijiandaa kwa kujadili kanuni za wasaka hifadhi barani humo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaka haki na maslahi ya watoto vipatiwe kipaumbele.

Mkurugenzi wa UNICEF, Geneva, Uswisi, Noala Skinner amesema wanataka kanuni mpya zihakikishe uamuzi wa kumpatia mtoto hifadhi unapatikana haraka ili kuepusha mtoto kukumbwa na hatari, tofauti na sasa ambapo inachukua miezi 11 tangu mtoto kuwasili na kubaini ni wapi ombi lake limekubaliwa.

Halikadhalika wanapendekeza ndani ya saa 72 mtoto afahamishwe haki yake ya kuomba hifadhi iwe yuko peke yake au hata anaambatana na ndugu au jamaa.

Kanuni mpya tarajiwa zitabainisha ni nchi gani inaweajibika kuzingatia maombi ya hifadhi ya kimataifa kutoka kwa wahamiaji, maombi yatakayowasilishwa katika nchi yoyote ya Ulaya.

Mjadala huo wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya na bunge unafanyika huku watoto zaidi ya 400,000 walioomba hifadhi Ulaya kati ya Januari na Novemba mwaka jana wakiwa hawafahamu hatma yao.

Photo Credit
Wakimbizi wanaokimbilia Ugiriki.Picha:UNICEF