Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM Yemen asihi pande zote zishiriki mazungumzo

Mjumbe wa UM Yemen asihi pande zote zishiriki mazungumzo

Pakua

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, ametoa wito kwa pande zote nchini Yemen zishiriki mazungumzo ya amani kwa nia nzuri, kufuatia ujumbe wa serikali kusitisha ushiriki wake katika mazungumzo hayo.

Licha ya kuwepo mazingira mazuri katika siku chache zilizopita, ujumbe wa serikali ulisitisha ushiriki wake katika mazungumzo ya wazi, kwa sababu ya ripoti zilizopkelewa kutoka Amran, Yemen.

Katika taarifa kwa vyombi vya habari, Bwana Cheikh Ahmed amesema kwamba anaelewa sababu zilizopelekea uamuzi huo wa upande wa serikali, lakini akatoa wito kwa pande zote zishiriki kwa nia nzuri na kudhihirisha busara wanaposhiriki mazungumzo hayo ya amani.

Akikutana na waandishi wa habari leo Jumatatu jijini New York, msemaji wa Katibu Mkuu, Stephane Dujarric, amekariri ujumbe wa Bwana Cheikh Ahmed...

“Amesema kwamba masuala yote yanayozua utata yanapaswa kujadiliwa kwenye meza ya mazungumzo kwa uwazi, ili kufikia makubaliano ya kina. Amesema pia kuwa anashirikiana na kamati ya kurejesha utulivu na uratibu, na kupitia kamati za mashinani ili kuchunguza ukiukaji wa sitisho la uhasama.”

Photo Credit
Mzozo wa Yemen unasababisha mateso kwa wakazi ikiwemo watoto.(Picha:WFP/Yemen)