Skip to main content

Ban akaribisha kurejea kwa Machar Juba kama Makamu wa kwanza wa Rais

Ban akaribisha kurejea kwa Machar Juba kama Makamu wa kwanza wa Rais

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha kurejea kwa Riek Machar Juba na kuapishwa kwake kama Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini, akisema hatua hiyo inafungua ukurasa mpya wa kutekeleza makubaliano ya amani.

Katika taarifa msemaji wake, Stephanne Dujarric amesema Ban ametoa wito serikali ya mpito ya muungano wa kitaifa iundwe mara moja, akipongeza juhudi za mwenyekiti wa kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kufanya tathmini, Rais wa zamani, Festus Mogae, na Mwakilishi mwandamizi wa Muungano wa Afrika (AU), Alpha Oumar Konaré.

"Katibu Mkuu ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lifanye kazi kwa karibu na IGAD, na Baraza la Usalama la AU, katika kupigia chepuo usaidizi wote unaohitajika kwa mchakato wa amani."

Photo Credit
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric. (Picha:UM/Maktaba/Evan Schneider)