Skip to main content

Ustawi wa watoto wakwazwa na ukosefu wa ulinzi wa kijamii: UNICEF

Ustawi wa watoto wakwazwa na ukosefu wa ulinzi wa kijamii: UNICEF

Pakua

Matumizi madogo katika huduma za kijamii, ukosefu wa ulinzi wa kijamii na mipango vinakwaza ustawi wa watoto Ulaya ya Kati na Mashariki, ukanda wa Caucasus na Asia ya Kati imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF.

Ripoti hiyo inayoitwa Ulinzi wa kijamii kwa haki za watoto  iliyozinduliwa leo inasema kuwa watoto hunufaika zaidi nchi zinapowekeza katika ulinzi wa kijamii.

Ikijumuisha ushahidi wa hivi karibuni kuhusu mwenendo wa wadau wa mabadiliko katika umasikini na madhara ya ulinzi wa kijamii ripoti imengazia  nchi 30 katika ukanda huo.

UNICEF katika ripoti hiyo inaangazia changamoto kuu ambazo ukanda unakabiliana nazo katika kutimiza mahiataji  ya ulinzi wa kijamii kwa watoto.

Photo Credit
Watoto Sudan Kusini ambako mzozo unatia maisha na ustawi wao mashakani.(Picha:UN/JC McIlwaine)