Ugonjwa wa kisukari na athari zake

Ugonjwa wa kisukari na athari zake

Pakua

Tarehe saba Aprili ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya afya. Siku hii inayoratibiwa na shirika la afya ulimwenguni WHO, hutumiwa kuhamasisha umuhimu wa afya kwa watu ambapo  mwaka huu imejielekeza katika ugonjwa wa Kisukari ikiwa na kauli mbiu Shinda Kisukari

Kwa mujibu wa WHO idadi ya watu wanaoishi na kisukari imeongezeka takribani mara nne tangu mwaka 1980 na kufikia watu wazima milioni 422 wengi wao wakiwa ni wakazi wa nchi zinazoendelea.  WHO inataka hatua zichukuliwe ikitaja sababu kubwa ya ongezeko hili ni pamoja na unene wa kupindukia.

WHO imesema lazima serikali zichukue hatua kudhibiti kasi ya ugonjwa wa kisukari kwa kuhakikisha vifo vinavyozuilika kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza vinapunguzwa kwa asilimia 30 ifikapo mwaka 2030.

Ili kudhihirisha kauli hiyo ya WHO ya kuongezeka kwa ugonjwa wa Kisukari, tunakupeleka nchini Uganda ambako John Kibego amekuwa akifuatailia mwenendo wa ugonjwa huo hususani huduma za afya kwa wagonjwa.

(KIBEGO PACKAGE)

Photo Credit
Hapa ni vipimo vya kisukari ambayo inaweza kutokea wakati wa uja uzito.(Picha:WHO/PAHO/Sebastián Oliel)