Ban abughudhiwa na kuzuka upya mapigano ya Nagorno-Karabakh.

Ban abughudhiwa na kuzuka upya mapigano ya Nagorno-Karabakh.

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anabughudhiwa na taarifa za hivi karibuni za uvunjaji wa kiwango kikubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda ukanda wa machafuko wa Nagorno-Karabakh. Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban amesikitishwa zaidi na matumizi ya silaha nzito na idadi kubwa ya majeruhi wakiwamo raia. Amezitaka pande zote kukomesha hima mapigano, kuheshimu makubaliano ya usitishwaji wa mapigano na kuchukua hatua za dharura za kutoendelea kwa machafuko. Ban amekariri uungwaji mkono kwa kundi la OSCE Minsk, na pande zote zinazofanya kazi ya kusaka kutuliza hali ya mzozo huo hatari na kwa kusaka amani kwa majadiliano.

Photo Credit