Né So,,,ni wimbo wa Rokia Traoré wazungumzia wakimbizi kwa UNHCR

Né So,,,ni wimbo wa Rokia Traoré wazungumzia wakimbizi kwa UNHCR

Pakua

Wakati ambapo idadi ya wakimbizi duniani kote imezidi milioni 60, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeteua mwimbaji maarufu wa Mali, Rokia Traoré, kuwa Balozi mwema wa shirika hilo kwa ukanda wa Afrika Magharibi na Kati.

Bi Traoré ambaye amekuwa akishirikiana na UNHCR katika kuelimisha jamii kuhusu suala la wakimbizi, amemulika umuhimu wa kurudi nyumbani kwa wakimbizi hao katika wimbo mpya alioutoa hivi karibuni.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

Photo Credit
Mtunzi na mwimbaji nyota wa muziki kutoka nchini Mali Rokia Traoré.(Picha: UNHCR/Video capture)