Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini CAR, sasa ni wakati wa kuimarisha mamlaka za serikali: Ladsous

Nchini CAR, sasa ni wakati wa kuimarisha mamlaka za serikali: Ladsous

Pakua

Akihitimisha ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous amewaelezea waandishi wa habari mjini Bangui matumaini yake kuhusu mwelekeo wa kisiasa nchini humo.

Amesema amefurahia sana na kuapishwa kwa rais mteule Faustin Archange Touadéra, akisema hatua hiyo ni mwisho wa utaratibu wa mpito na mwanzo wa wakati wa kuleta maendeleo nchini.

Bwana Ladsous amesisitiza umuhimu wa kutekeleza mchakato wa kujisalimisha kwa waasi na kuimarisha mfumo wa sheria ili kupambana na ukwepaji wa sheria, akisema la msingi ni.

(Sauti ya Ladsous)

“ Kuhakikisha Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo imeshuhudia mizozo mingi katika miaka iliyopita sasa inakwepa mzunguko huo wa mizozo. Na kwamba tunaweza kutatua matitizo ya misingi kwa uendelevu, na tatizo la kwanza ni udhaifu wa serikali, kama taasisi lakini pia mfumo wa fedha, ushuru na maendelo…”

Photo Credit
Hervé Ladsous, mkuu wa DPKO, pamoja na Parfait Onanga-Anyanga mkuu wa MINUSCa, akikutana na jamii nchini CAR. Picha kutoka video ya MINUSCA.