Skip to main content

Watu wanaohitaji misaada maeneo yaliyozingirwa Syria bado hawaipati:UM

Watu wanaohitaji misaada maeneo yaliyozingirwa Syria bado hawaipati:UM

Pakua

Nchini Syria maelfu tya watu ambao wanahitaji misaada ya haraka bado haiwafikii katika baadhi ya maeneo yaliyozingirwa umesema Umoja wa mataifa Alhamisi. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Kwa mujibu wa Jan Egeland, ambaye ni mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria , kuna hali ya taharuki kwamba kazi ya awali ambayo ilisaidia misafara ya misaada kuwafikia watu wanaoihitaji  nchini Syria sasa imepungua.

Akizungumza mjini Geneva kwenye kikao wakuu wa kikosi kazi cha masuala ya kibinadamu kuhusu Syria, bwana Egeland ameonya kwamba sasa  kufikisha misaada kwenye jamii za Syria zinazozingirwa ni shinikizo . Ameongeza kuwa kuna maeneo matatu nje ya Damascus ambayo bado hayafikiki kati ya maeneo 18 yanayozingirwa.

(SAUTI YA EGELAND)

“Bado hatuja[pata fursa  kabisa ya kuingia katika eneo la Duma, Darayya na mashariki mwa  Harasta. Duma, ni eneo kubwa watu Zaidi ya 90,000 wanahitaji msaada. Darayya, ni eneo ambalo hali ni mbaya sana kwa raia wachache waliosalia hapo

Hadi sasa Umoja wa mataifa na wadau wake mwaka huu wameweza kuwafikia watu zaidi ya 400,000 katika maeneo yaliyozingirwa ambayo ni magumu kufikika na maeneo mengine ambayo yana hali mbaya ya kibinadamu.

Photo Credit
Huyu ni Lina mkimbizi kutoka Syria aliyekimbilia Lebanon.(Picha© UNHCR/A.McConnell)