Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumu wa afya wananufaisha kwa afya, uchumi na ajira- WHO

Wahudumu wa afya wananufaisha kwa afya, uchumi na ajira- WHO

Pakua

Kukuza fursa za ajira kwa wahudumu wa afya kunaweza kuimarisha afya na uhakika wa afya bora, kuchagiza ukuwaji wa uchumi na kuwezesha wanawake na wasichana, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Margaret Chan, baada ya mkutano wa kwanza wa Kamisheni kuhusu ajira katika sekta ya afya na ukuaji wa uchumi, ambao umefanyika jijini Lyon, Ufaransa.

Dkt. Chan amesema ajira katika sekta ya afya zinaweza kupunguza mapengo yanayozidi kupanuka ya tofauti za kiuchumi na fursa, akitoa wito kwa watunga sera kubadilisha mtazamo wao, ili sekta ya afya isionekane kama inayofuja rasilmali, bali izingatiwe kama chanzo cha fursa nyingi.

Ongezeko la idadi ya watu pamoja na mabadiliko ya mienendo ya maradhi na kiuchumi yanatarajiwa kuchangia kufunguliwa kwa fursa mpya milioni 40 za ajira katika sekta ya afya ifikapo mwaka 2030, hususan katika nchi zenye kipato cha wastani na zenye kipato cha juu kiuchumi.

Wakati huo huo, inakadiriwa kuwa kutakuwa na upungufu wa wahudumu wa afya milioni 18 katika nchi za kipato cha chini, na hivyo kutatiza kutimizwa kwa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Photo Credit
Elvina-Mkunga Tanzania. Picha@UNFPA