Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watoto 250,000 wameathirika na vita Colombia tangu 2013:UNICEF

Zaidi ya watoto 250,000 wameathirika na vita Colombia tangu 2013:UNICEF

Pakua

Zaidi ya watoto 250,000 wameathirika na vita Colombia tangu tangu kuanza kwa mazungumzo ya amani baina ya serikali na kundi kubwa la upinzani la (FARC-EP) miaka mitatu iliyopita  imesema ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyotolewa Jumatatu.

Inakadiriwa watoto 1,000 wametumiwa vitani na makundi yenye silaha yasiyo ya serikali katika kipindi hicho kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na Umoja wa mataifa na serikali.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Colombia Roberto De Bernardi amesema wakati majadiliano ya amani yakiendelea kumaliza nusu karne ya vita nchini Colombia ni muhimu saana kuyapa kipaumbele maslahi na ulinzi wa watoto.

Ameongeza kuwa hatuna mtoto Colombia mbaye leo hii anajua inakuwaje kuishi katika nchi ya amani, hivyo imewadia wakati wa kugeuza ukurasa huo.

Ripoti hiyo “utoto katika wakati wa vita” imesema Zaidi ya watoto 230,000 wametawanywa na vita hivyo, 75 wameuawa, huku wengine 130 wakijeruhiwa na wapatao 180 kuwa wahanga wa ukatili wa ngono kati yam waka 2013 na 2015.

Photo Credit
Watoto wakimbizi wa ndani nchini Colombia. Picha ya Umoja wa Mataifa/Mark Garten.