Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inawasaidia wahamiaji Wanigeria waliokwama kutoka Sudan:

IOM inawasaidia wahamiaji Wanigeria waliokwama kutoka Sudan:

Pakua

Wahamiaji 42 raia wa Nigeria waliokuwa wamekwama Sudan, wamerejea nyumbani kufuatia msaada wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM.

Miongoni mwao ni wanawake 31 na watoto 19.

Wahamiaji hao walisafiri kwa ndege hadi uwanja wa kimataifa wa Kano nchini Nigeria wakitokea mjini Khartoum, Sudan.

Operesheni hiyo ilikuwa ni sehemu ya mradi wa IOM unaofadhiliwa na serikali ya Norway wa kuboresha ulinzi na kuimarisha uelewa wa hatari inayowakabili wahamiaji nchini Sudan.

Wengi wa wahamiaji hao wameishi Sudan kati ya mwaka mmoja hadi mitatu na wamekaribia ufukara kutokana na kuishi mitaani huko Khartoum, wakitegemea kufanya kazi za vibarua na kuombaomba.

Photo Credit
IOM yasaidia waNigeria waliokwama nchini Sudan.(Picha:IOM)