Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 70 ya Redio ya Umoja wa Mataifa

Miaka 70 ya Redio ya Umoja wa Mataifa

Pakua

Radio! Tarehe 13 mwezi Februari imetengwa kuwa siku muhimu ya kuadhimisha chombo hiki cha upashaji habari kinachoendelea kuongoza kwa kutegemewa zaidi kote ulimwenguni! Siku hii imetengwa kwa kuzingatia kuwa Radio ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa kupitia azimio la Baraza kuu la Umoja wa Mataifa la tarehe 13 Februari mwaka 1946! Kwa mantiki hiyo maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Radio duniani yanaenda sambamba na miaka 70 ya kuanzishwa kwa Radio ya Umoja wa Mataifa!

Hivyo basi makala hii itaangalia Radio ya Umoja wa Mataifa ilipotoka, ilipo na inapoelekea! Je teknolojia inatowesha nafasi ya radio? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii ya wiki!

Photo Credit
UN Photo.