Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID redio na wajibu wake katika mizozo Sudan

UNAMID redio na wajibu wake katika mizozo Sudan

Pakua

Siku ya radio duniani hudhimishwa tarehe 13 Februari kila mwaka, mwaka huu inaaadhimishwa sambamba na miaka 70 ya redio ya Umoja wa Mataifa huku umuhimu wa redio katika majanga ikiwa ni maudhui mwaka huu. Nchini Sudan hususani katika jimbo la Darfur redio ya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika jimboni humo UNAMID pamoja na mambo mengine inatekeleza wajibu muhimu wa kuzipatia fursa za kushiriki kwenye majadiliano pande kinzani ili kupata amani ya kudumu. Mkuu wa redio ya UNAMID Jumbe Omari Jumbe amemweleza Joseph Msami katika mahojiano maalum kuwa wajibu huo pamoja na mambo mengine huokoa maisha ya watu.

Photo Credit
Watu wenye ulemavu wakipokea redio huko Zalengei. Picha:UNAMID/Abdulrasheed Yakubu