Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMF yatiwa hofu na kasi ndogo dhidi ya rushwa huko Ukraine

IMF yatiwa hofu na kasi ndogo dhidi ya rushwa huko Ukraine

Pakua

Shirika la fedha duniani, IMF limeeleza wasiwasi wake juu ya kasi ndogo ya kuimarisha utawala bora na kukabiliana na rushwa nchini Ukraine.

Mkurugenzi Mkuu wa IMF Christine Lagarde amesema hayo katika taarifa yake iliyotolewa leo.

Amesema kasi hiyo inatia shaka uwezekano wa kuendeleza miradi inayoungwa mkono na shirika hilo nchini Ukraine akisema kuwa siyo tu kuendelea bali pia kufanikiwa.

Bi. Lagarde amesema Ukraine iko hatarini kurejea kwenye mwelekeo wa sera za uchumi zisizo na mashiko ambazo zimekuwa sehemu ya historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo.

Kwa mantiki hiyio ametaka uongozi wa Ukraine kuchukua hatua sasa ili kurejesha nchi hiyo kwenye mwelekeo wa matumaini wa marekebisho ya uchumi.

Photo Credit
Mkurugenzi Mkuu wa IMF Christine Lagarde. Picha:UNIFEED Video Capture