Skip to main content

Idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya kila siku yazidi mara 10

Idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya kila siku yazidi mara 10

Pakua

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM limekadiria kuwa zaidi ya wahamiaji na wakimbizi 76,000 wamewasili barani Ulaya kwa njia ya bahari katika wiki sita za kwanza za mwaka huu wa 2016.

Katika taarifa yake IOM imesema kiwango hicho ni sawa na watu Elfu Mbili kila siku, idadi ambayo ni ongezeko la wastani wa mara 10 ikilinganishwa na mwaka jana.

Ongezeko hilo limeenda sambamba na idadi ya watu waliofariki dunia au kupotea ambayo ni 400 tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo wasafiri wanavuka bahari ya Mediteranea kutoka Afrika Kaskazini au Uturuki.

Kwa mujibu wa IOM wahamiaji na wakimbizi hao wanawasili Ugiriki na Italia ambapo sasa huko Macedonia shirika hilo linasaidiana na mamlaka za mji wa Skopje kuweka vifaa vya joto kwenye makazi ambako nako wahamiaji hao wanawasili.

Photo Credit
Picha:IOM/MOAS.eu/Jason Floria