Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Prof. Murenzi wa Rwanda miongoni mwa wataalam wa kuwezesha teknolojia katika SDGs

Prof. Murenzi wa Rwanda miongoni mwa wataalam wa kuwezesha teknolojia katika SDGs

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuwa amemteua Prof. Romain Murenzi wa Rwanda, kuwa miongoni mwa wataalam kumi watakaosaidia katika utaratibu wa uwezeshaji wa teknolojia, ambao ulizinduliwa katika mkutano wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, mnamo Septemba 25, 2015.

Wengine waliotajwa katika kundi la wataalam hao kumi ni Bw. Peter Bakker wa Uholanzi, Prof. Elmer William Jr Colglazier wa Marekani, Dkt. Myrna Cunningham wa Nicaragua, Bi. Elenita Daño wa Ufilipino, Dkt. Hayat Sindi wa Ufalme wa Saudia, Dkt. Paulo Ernani Gadelha Vieira wa Brazil, Dkt. Heide Hackmann wa Afrika Kusini, Prof. Nebojsa Nakicenovic wa Montenegro na Prof. Xiaolan Fu wa Uingereza.

Profesa Murenzi, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha World Academy of Science.

Utaratibu wa uwezeshaji wa teknolojia (TFM) uliwekwa kwa minajili ya kusaidia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Utaratibu huo unajumuisha timu ya pamoja ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi (STI) inayoleta pamoka wataalam kutoka mashirika 25 ya Umoja wa Mataifa; mkutano wa kila mwaka wa wadau kuhusu sayansi, teknolojia na uvumbuzi; na jukwaa la mtandao wa intaneti ambalo litatoa taarifa kuhusu mikakati, utaratibu, na programu zilizopo za sayansi, teknolojia na uvumbuzi.

Photo Credit
Picha@WIPO