Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP, ZAYED kutenegeza kitabu kuhusu uchumi rafiki kwa mazingira

UNEP, ZAYED kutenegeza kitabu kuhusu uchumi rafiki kwa mazingira

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP na taasisi ya kimataifa ya mazingira iitwayo Zayed leo wametia saini makubaliano ya kuzalisha kitabu cha kiada cha kimataifa kuhusu ujumuishwaji wa uchumi unaozingatia maizingira.

Makubaliano hayo yamesainiwa  na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner na mwenyekiti wa kamati kuu ya Zayed Dk Mohammed Ahmed bin Fahad ambapo mpango huo utaendeshwa  hadi mwezi Februari mwaka 2017 katika makao makuu ya UNEP mjini Nairobi Kenya.

Taasissi ya Zayed inayoratibu tuzo yenye thamani  kubwa zaidi ikiwa ni  dola milioni moja, itachangia dola laki moja katika utungwaji wa kitabu hicho cha kiada amabacho kitatoa mtizamo wa jumla wa uchumi unaozingatia mazingira na jukumu lake katika kupigia chepuo maendelo endelevu.

Photo Credit
Achim Steiner, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP (Picha@UN-Radio)