Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wanaokimbilia Ulaya hatarini kwa unyanyasaji wa kijinsia:UNHCR,UNFPA,WRC

Wanawake wanaokimbilia Ulaya hatarini kwa unyanyasaji wa kijinsia:UNHCR,UNFPA,WRC

Pakua

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, shirika la idadi ya watu duniani UNFPA na tume ya wanawake wakimbizi WRC wanatiwa hofu na hatari zinazowakabili wanawake na wasichana wakimbizi na wahamiaji wanaohamia Ulaya.

Mashirika hayo yamesema msimu mkali wa baridi inamaanisha sio watu wengi wanaochukua safari ya hatari kupitia bahari kuingia Ulaya hivi sasa ikilinganishwa na miezi iliyopita. Hata hivyo bado kuna wastani wa watu 200 wanaowasili kila siku.

Mashirika hayo yamesema na wakati serikali zikizidi kukaza kamba katika kulinda mipaka yake , maeneo ambako watu wanafikia na kupokelewa kunaweza kufurika tena  na hivyo kuongeza hatari kwa wanawake na wasichana.

UNHCR, UNFPA WRC  wamefanya tathimini ya pamoja kuhusu hatari inayowakabili wanawake na wasichana wahamiaji na wakimbizi nchini Ugiriki na na Jamhuri ya Yugoslavia ya zamani ya Macedonia mwezi Novemba mwaka jana.

Tathmini imebaini kwamba wanawake wanaosafiri peke yao, au na watoto, akian mama wanaonyonyesha, wasichana wadogo, watoto wasio na wazazi wanawake na wanaume wazee na wanawake wajawazito ni miongoni mwa watu walio katika hatari na wanahitaji kulindwa.

Wameongeza kuwa wanawake wengi na wasichana wahamiaji na wakimbizi wameshakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono, kwenye nchi watokako, wakiwa njiani n ahata wakiwsili Ulaya.

Photo Credit
Wakimbizi wa Syria(Picha ya UNHCR)