Dola bilioni 1.3 zahitajika kusaidia watu milioni 5.1 Sudan Kusini:OCHA

Dola bilioni 1.3 zahitajika kusaidia watu milioni 5.1 Sudan Kusini:OCHA

Pakua

Mpango wa kusaidia masuala ya kibinadamu Sudan Kusini kwa mwaka 2016 uliozinduliwa leo rasmi mjini Juba umeomba dola bilioni 1.3 ili kukabiliana na mahitaji ya lazima ya kuokoa maisha kwa watu zaidi ya milioni tanonchini humo.

Jumla ya mashirika 114 ya misaada ya kibinadamu yakiwemo ya kimataifa, yasio ya kiserikali yaani NGOs na mashirika ya Umoja wa Mataifa yana miradi yake katika mpango huo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mratibu wa masuala ya kibinadamu Sudan Kusini, Eugene Owusu, amesema mashirika ya masuala ya kibinadamu yanajitahidi kuongeza nguvu na uwepo wao ili kuwafikia watu wengi zaidi kadri inavyowezekana.

Ameongeza kuwa ombi lao ni lazima lifadhiliwe kikamilifu na linawakilisha kiwango cha chini cha mahitaji yanayotakiwa kukidhi mahitaji ya haraka na ya lazima na mahitaji hayo hayawezi kutotimizwa. Ameongeza kuwa changamoto wanayokabiliana nayo ni kubwa lakini hawatakata tamaa.

Mwaka jana wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu walifanya kazi bila kuchoka kuwafikia Zaidi ya milioni 4 waliokuwa wanahitaji msaada wa kuokoa maisha.

Photo Credit
Usambazaji wa misaada kwa wakimbizi nchini Sudan Kusini.(Picha:UM/JC McIlwaine)