Hassen Ebrahim Mussa ndiye kamanda mpya wa UNISFA

Hassen Ebrahim Mussa ndiye kamanda mpya wa UNISFA

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon leo ametangaza uteuzi wa Meja Jenerali Hassen Ebrahim Mussa wa Ethiopia kama kamanda mpya wa vikosi vya usalama vya muda vya Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Abyei (UNISFA).

Anachukua nafasi ya Luteni Jenerali  Birhanu Jula Gelalcha wa Ethiopia ambaye atahitimisha muda wake tarehe 20 ya mwezi huu. Katibu Mkuu amemshukuru Gelalcha kwa uongozi wake shupavu na utendaji wake wa kazi akiongoza vikosi hivyo.

Meja Jenerali Mussa ana uzoefu mkubwa na vikosi vya Ethiopia , na hivi sasa ni mkuu wa kituo cha uratibu wa kulinda amani kwenye majeshi ya Ethiopia. Jenerali huyo alihitimu  katika chuo cha makamanda wa jeshi cha Ethiopia mwaka 2005 na ameshika nyadhifa mbalimbali jeshini na mwaka 2010-2011 alikuwa kamanda wa moja ya vitengo vya UNAMID.

Meja Jenerali Mussa ana shahada ya uzamili ya biashara aliyoipata katika chuo kikuu huria nchini Uingereza. Alizaliwa mwaka 1966, ameoa na ana watoto wanne.

Photo Credit
Picha:Martine Perret