Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yaomba dola milioni 800 za usaidizi Syria na maeneo ya Palestina yaliyokaliwa

UNRWA yaomba dola milioni 800 za usaidizi Syria na maeneo ya Palestina yaliyokaliwa

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limetangaza ombi la changisho la dola milioni 817 ili kuwasaidia wakimbizi wa Syria walioko nchini Syria na maeneo ya Palestina yaliyokaliwa, wakati maeneo hayo yakiendelea kukumbwa athari za mzozo, kukaliwa na vizuizi.

Wengi wa raia wa Palestina 450,000 walioko nchini Syria wamelazimika kuhama, na asilimia 95 yao hutegemea usaidizi wa UNRWA.

Maelfu bado wamenaswa katika maeneo yanayoshuhudia vita, wakikabiliwa na hali mbaya ya maisha, huku makumi ya maelfu yaw engine wakiwa wamekimbilia Lebanon na Jordan ambako licha ya ukarimu wa nchi hizo, bado wanakabiliwa na kutelekezwa na kukata tamaa.

Katika maeneo ya Palestina yaliyokaliwa, wakimbizi hao wanaendelea kukabiliwa na madhara ya maeneo hayo kukaliwa kwa kipindi cha takriban miaka 50 sasa na vizuizi vya muongo mmoja.

Photo Credit
Picha:UNRWA