Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza Sri Lanka kwa mwaka mmoja wa kipindi cha mpito

Ban aipongeza Sri Lanka kwa mwaka mmoja wa kipindi cha mpito

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amempongeza Rais wa Sri Lanka, Maithripala Sirisena, serikali na watu wa nchi hiyo kwa kutimiza mwaka mmoja wa serikali ya mpito wa kisiasa.

Ban ametiwa moyo na serikali kujidhatiti katika ajenda ya mabadiliko  ambayo yana lengo la kuhakikisha amani ya kudumu , utulivu na mafanikio kwa watu wa Sri Lanka.

Katibu mkuu anatambua hatua za awali zilizochukuliwa na serikali kuimarisha utawala bora, hatua za awali za maridhiano na utekelezaji azimio la baraza la haki za binadamu la Oktoba 2015.

Amewataka kuendelea na mchakato katika maeneo hayo muhimu na kuhimiza haja ya kujumisha pande zote katika mchakato wa mjadala wa kushughulikia masuala ya mpito ya haki. Pia amepongeza uongozi wa Sri Lanka kwa juhudi zake za kutataka kubadili ndoto za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya 2030 kuwa kweli.

Photo Credit
Msichana nchini Sri Lanka.(Picha:UM/Evan Schneider)