Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sigrid Kaag akutana na waziri mkuu wa Lebanon

Sigrid Kaag akutana na waziri mkuu wa Lebanon

Pakua

Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Lebanon Bi Sigrid Kaag leo Alhamisi amekutana na waziri mkuu wa Lebanon Tammam Salam aliporejea kutoka Saudi Arabia kwenye  ziara ya kikazi.

Bi Kaag amempa taarifa waziri mkuu huyo kuhusu mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Saudia Adel Al-Jubeir na maafisa wengine wa serikali. Majadiliano yake na viongozi wa Saudia yalijikita kwenye masuala ya siasa, usalama na urejeshaji wa utulivu Lebanon na katika kanda nzima.

Waziri mkuu wa Lebanon na Bi Kaag wamejadili juhudi za kuchagiza utulivu Lebanon ikiwemo azimio linalohitajika kumaliza pengo la urais, pia wamegusia maandalizi ya mkutano mkubwa unaotarajiwa karibuni wa wahisani wa Syria.

Photo Credit
Sigrid Kaag akikutana na wakimbizi wa Syria nchini Lebanon. Picha ya UN/maktaba