Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utengenezaji mitumbwi huko Mwanza wakwamua maisha ya vijana

Utengenezaji mitumbwi huko Mwanza wakwamua maisha ya vijana

Pakua

Lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa mwezi Septemba mwaka huu linataka umaskini uwe umetokomezwa ifikapo mwaka 2030. Umaskini umekuwa ni mwiba kwa wakazi wengi hususan katika nchi zinazoendelea na matokeo yake wakazi wake hususan wanawake, vijana na watoto kushindwa kukidhi mahitaji yao ya msingi ikiwemo yale ya kijamii. Ni kwa mantiki hiyo harakati za kutokomeza umaskini na kuinua kipato cha jamii zinashika kasi kila uchao, mathalani huko Mwanza nchini Tanzania ambako vijana sasa wamechukua hatua. Je ni nini wanafanya? Ungana na Martin Nyoni wa Radio washirikia, Radio SAUT FM kutoka nchini humo.

Photo Credit
Uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria. Picha kutoka video ya UNIFEED.