Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu bora ni changamoto kwa wakimbizi Uganda

Elimu bora ni changamoto kwa wakimbizi Uganda

Pakua

Nchini Uganda, katika wilaya ya Kiryandongo iliyoko katikati mwa nchi, idadi ya wakimbizi wanaoishi kambini imeongezeka sana tangu kuibuka kwa mzozo wa Sudan Kusini, Disemba, mwaka 2013, uliosababisha watu wengi kukimbia mapigano.

Kwa ujumla, ni zaidi ya wakimbizi 500,000 waliotafuta hifadhi nchini humo kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR, wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.

Miongoni mwa changamoto zilizopo kambini ni upatikanaji wa huduma za elimu, madarasa yakiwa yamejaa na kupungukiwa vifaa vya kusomea . Kulikoni? Ungana na John Kibego katika makala hii.

Photo Credit
Watoto wakimbizi nchini Uganda wakisoma chini ya mti. Picha ya UNHCR.