IOM yasaidia serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu

IOM yasaidia serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu

Pakua

Nchini Tanzania, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesaidia wahamiaji 54 wa Ethiopia kurudi makwao, kwa ushirikiano no idara ya uhamiaji ya serikali ya Tanzania.

Wakimbizi hao walikuwa wamefungwa na serikali ya Tanzania kwa zaidi ya miezi minne kwa sababu ya kuingia nchini humo kinyume cha sheria na hivyo kukosa nyaraka halali za kusafiri.

Miongoni mwao ni vijana sita wenye umri wa chini ya miaka 18, ambao walisafiri bila wazazi wao.

Mradi huu ambao ulilenga kuwarejesha makwao na kuwapatia huduma za msingi umefadhiliwa na serikali ya Japan kupitia ubalozi wake nchini Tanzania.

Charles Mkude kutoka IOM amesimamia mradi huo nchini Tanzania na amefafanau kwa kina alipohojiwa na Priscilla Lecomte wa Idhaa hii. Kwanza anaeleza lengo la mradi huu.

Photo Credit
Wahamiaji kutoka Ethiopia wakirudi kwao. Picha ya IOM.